UJUMBE MUHIMU KUTOKA KWA MHE. BALOZI MULAMULA

21 February 2014

Kwa Viongozi wote wa Jumuiya ya Watanzania - Marekani,

Salaam!!!

Natumaini wote hamjambo na  mnaendelea vema na shughuli zenu za kila siku, sisi huku Washington, DC pia hatujambo, tunamshukuru Mungu.

Naomba kuwafahamisha wote kwamba Mhe. Balozi Liberata Mulamula ametoa siku maalum JUMANNE ya kwanza ya kila mwezi ya wale watakaopenda kuonana naye/kuzungumza kwa njia ya simu, iwe kwa salaam/kujitambulisha au kwa mazungumzo ya kuendeleza Taifa letu, utaratibu huu utaanza rasmi mwezi wa Februari, 2014.

Unaweza kupiga simu 202-884-1081 au 202-939-6125 Ext. 181/184 ili kuweza kuweka miadi hiyo kwa siku hiyo. Pia unaweza kuja Ubalozini kwa nafasi yako na kama Mhe. Balozi atakuwepo na akiwa na nafasi muafaka basi ataweza kukuona.  Tunaomba pia muwafahamishe na wengine kuhusu jambo hili.

Taarifa maalum itawekwa kwenye website yetu ya Ubalozi, pamoja na blogs zote ambazo zinasomwa kwa wingi na Watanzania wote waishio hapa Marekani.

Ahsanteni na kazi njema!

Wenu katika ujenzi wa Taifa,
Rosemary
Ofisi ya Balozi
202-884-1081

Read 2283 times

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.