25 February 2014
Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.
 
Misaada  toka kwa  Bi Gladness Sariah wa Uingereza,  Dar es salaam kwaNorah SilverBoutique
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwakilisha msaada toka kwa familia ya mama Masawe wa DSM kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha NURU kilichopo Uyole, mkoani Mbeya.
-----------------------
Kituo cha Mtandao wa kijamii cha Mbeya Yetu (www.mbeyayetu.blogspot.com) kimepokea Misaada mbalimbali kutoka kwa wasamaria wema kwa ajili ya Kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole Jijini Mbeya na  Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.
Msaada wa kwanza ulipokelewa hivi karibuni wenye thamani ya shilingi Laki Moja kutoka Familia ya Masawe wa Dar es salaam kwa ajili ya kituo cha Nuru ambapo Mbeya yetu iliuwasilisha kama ulivyo.
Mbali na msaada huo pia Mtandao huu ukishirikiana na mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Jijini Dar es salaam wa www.issamichuzi.blogspot.com ulipokea kutoka kwa Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ambaye alitoa maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto.
Aidha katika kuonesha wengi wameguswa na tukio la Mwanamke huyo kujifungua watoto wanne  ambao wanaendelea vizuri, pia Msamaria  mwema mwingine aliyejulikana kwa jina la  Dada Norah SilverBoutique toka Dar es salaam naye  ametoa Maziwa Lactogen makopo 24 pamoja na nguo ambavyo vimewasili salama katika ofisi ya Mbeya Yetu.
 Shukrani kwa Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza na ofisi za Michuzi Media Group (MMG) kuwezesha kufika kwa mizigo hii Mbeya.
Kutokana na kupokelewa kwa mizigo hiyo ambapo kituo cha Nuru kilikabidhiwa Katoni Mbili za Sukari, Sabuni na Biskuti pia Tunatarajia kuanza  safari ya kwenda huko Chiwanda Wilaya ya Momba Kilomita zaidi ya 260 toka Mbeya mjini kufikisha misaada ya Mama wa mapacha wanne. 
Hivyo ni wito wetu kwenu kuendelea kutuombea na kutuunga mkono katika safari hiyo ili tuweze kuifikisha salama mizigo hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia maendeleo ya Watoto hao ambapo watakuwa wameshatimiza mwezi mmoja na siku 24.
Tunawashukuru sana tena sana wote mliojitolea na Mungu awabariki sana. 
Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ama This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 
Nasi tutafikisha ubani wako. 
Wazee wa Kazi Serengeti Freight wametoa ofa ya 
kusafirisha bure misaada ya aina hii toka Uingereza.
Mbarikiwe sana Wazee wa Kazi.
23 February 2014

Mtanzania Elisha Bahunde jina maarufu Eric ambaye siku ya Jumamosi Feb 15, 2014 alipata ajali Jimbo la Indiana iliyopelekea kukatika kwa miguu yote miwili na mkono wa kulia na baadae kuhamishiwa Jimbo la Maryland kwa matibabu zaidi kwa sasa yupo University Of Maryland Medical Center iliyopo 22 S Greene St, Baltimore, MD Ghorofa ya 6 chumba # 8 na anatumia jina la Elisha Bahunde ama kweli hujafa hujaumbika na Mwenyezi Mungu ndiye mueza wa kila jambo ebu sikiliza mwenyewe video hiyo hapo chini na ujionee na picha pia tumekuekea video aliyoshiriki kwenye Kijiwe cha Ughaibuni ameva shati la njano na amekaa karibu na Ally Bambino

 

 Elisha Bahunde akiwa chumba # 8 ghorofa ya 6 alipolazwa tangia siku ya Jumatano Feb 19, 2014 alipoletwa Maryland kwa matibabu zaidi
 Elisha Bahunde au Eric akiwa hana miguu wa mkono kama picha inavyoonyesha.
 Rais wa Jumuiya DMV, Bwn. Idd Sandaly akiwa Hospitalini hapo kumjulia hali mgojwa
 Abdi Makeo amkimjulia hali Elisha Bahunde
 Said Mwamende akimjulia hali Bwn. Eric huku akilengwa na machozi
 Wanajumuiya waliofika kumjulia hali wakiwa hawaamini walichokiona.
Kutoka kushoto ni Abdi Makeo, Saidi Mwamende, Rais wa DMV Idd Sandaly na Jabir Jongo wakiwa chumba cha mapumziko baada ya kumaliza kumjulia hali Elisha Bahunde kwa jina lingine Eric
 

 

22 February 2014

DSCF2880Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw.Philemon Mollel akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga msaada wa Tani nne za unga  wenye thamani ya shilingi Milioni 4.2,baada ya wilaya yake kupata maafa yaliyotokana na mvu zilizoambatana na upepo mkali na kusababisha badhii ya watu kukosa nyumba za kuishi
DSCF2878Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga Arusha Philemon Mollel akiongea mbele ya wanakijiji(hawapo pichani)namna alivyoguswa na maafa hayo yaliyopelekea kutoa msaada huo huku kiwataka wafanyabishara,makampuni,watu binafsi kujitokeza kuwasaidia waanga wa maafa hao,mbali na msaada huo wa tani nne za unga pia alitoa shilingi Milioni moja kwaajili ya waanga
DSCF2861
DSCF2857Mkuu wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga akiwa na ugeni mzito kutoka kampuni ya Monaban ofisini kwake,lengo la ugeni huo nikutoa msaada wa chakula kwa waathirika wa maafa ya mvua
DSCF2858Mkurugenzi wa Monaban kushoto Philemon Mollel akiongelea namna alivyoguswa na maafa hayo ambayo yalisababisha baadhi ya watu kukosa makazi ,
DSCF2866Kina mama ambao ndio waathirika wa kubwa wa maafa hayo wakisubiria zoezi la kugawiwa chakula cha msaada 
DSCF2870Mtendaji wa kijiji Bi.Trea Ramadhani akitoa shukrani zake za dhati kwa mmiliki wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichipo Arusha
DSCF2872Afisa Tarafa Masama Bw.Nsajigwa Ndagile akisoma taarifa ya madhara yaliyotokana na mvua hiyo kuwa ni pamoja na kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,kubomolewa kwa kuta za nyumba na kuharibiwa kwa mazao hasa migomba hali iliyosababisha baadhi ya kaya kukosa mahali pa kulala hivyo kujihifadhi kwa majirani
DSCF2874Wanakijiji wakishuhudia msaada ulioletwa kijijini kwao 
DSCF2882Mkuu wa wilaya Novatus Makunga akimkabidhi msaada uliotolewa na kampuni ya Monaban ,mtendaji wa kijiji cha  kwa sadala Bi.Trea Ramadhani msaada uliogharimu zaidi ya milioni 4,Kushoto ni kaimu mkurugenzi Bw.Zabdieli Moshi
DSCF2883Mkuu wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga akitoa shukrani zake za dhati kwa mmiliki wa kiwanda cha Monaban kwa kuweza kuwaletea chakula cha msaada na kuwataka makampuni,mashirika na watu binafsi kuiga mfano wa Monaban kwa kuwasaidia waanga wa maafa yaliyotokana na mvua zilizoambatana na upepo mkali na kusababisha watu kukosa makazi hivi karibuni ktika wilaya yake
DSCF2886Mama ambaye ni muathirika wa maafa hayo akitoa shukurani zake kwa mkurugenzi wa kampuni ya Monaban kwa kuweza kuwakumbuka kipindi cha shida na kudai kuwa akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli
 
Nyumba ya familia ya Bibi Aziza Mohammed baada ya kuezuliwa paa
 Bibi Aziza Mohammed kama anavyooneka katika picha baada ya mvua kusababisha mafaa makubwa kwake hali iliyosababisha yeye kuishi chooni na mjuuku wake
DSCF2862DSCF2865Wanakijiji wakiwa wanashusha mifuko ya unga ndani ya gari.(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

TaWichita Login

Calendar

« June 2019 »
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
          1 2
3 4 5 6 7 8 9
10 11 12 13 14 15 16
17 18 19 20 21 22 23
24 25 26 27 28 29 30